Vinicius Junior atabiriwa Ballon D'or 2024

Nyota wa Real Madrid ya Hispania Vinicius Junior usiku wa jana Oktoba 22, 2024 aliushangaza ulimwengu wa Soka baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Borrusia Dortmund uwanja wa Santiago Bernabeu. Vini alifunga magoli matatu na kuiongoza Madrid kupata ushindi wa goli 5-2.

Mara ya mwisho Mchezaji kutoka Brazil kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Dunia  ilikuwa msimu wa 2006-2007 Ricardo Eziksen Leite 'Kaka' alishinda tuzo hiyo mbele ya  Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS