Harry Kane aweka rekodi nchini Ujerumani

Harry Kane Mshambuliaji wa Bayern Munich jana alifunga goli tatu hat-trick dhidi ya Stuttgat na kufikisha idadi ya hat-trick Sita tangu ajiunge na Bavarians kutokea Tottenham Hotspurs ya Uingereza. Kane anashikilia rekodi ya kuwa Mchezaji mwenye asili ya Uingereza aliyefunga goli nyingi zaidi kwenye ligi kuu nchini Ujerumani mbele ya Kevin Keegan, Jude Bellingham na Tony Woodcock.

Nahodha wa timu ya taifa ya England Harry Kane jana alifunga goli tatu dhidi ya Stuttgat na kuiwezesha Bayern Munich kureje kileleni mwa msimamo wa Bundesliga mbele ya RB Lepzig kwa tofauti ya magoli. Kane alifunga hat -trick na kumfanya afikishe idadi ya goli 13 katika michezo 10.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS