Moussa Camara unapaswa kutambua hii ni Tanzania

Moussa Camara Golikipa mpya raia wa Guinea alibeba matumaini makubwa ya Wana Msimbazi kwa kupata Mlinda Mlango ambaye anauwezo wa kucheza mpira kwa miguu yake. Katika michezo miwili mfululizo nyota huyo amefanya makosa ambaye yameigharimu klabu ya Simba alama 5 ambazo zinaweza kuwa alama muhimu kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu ambao timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi Karikaoo imeutafuta kwa misimu mitatu mfululizo bila mafanikio.
Moussa Camara amefanya makosa katika michezo miwili mfululizo ambayo yameiathiri timu ya Simba kwa kusababishia kudondondosha alama ambazo zinawapa faida Mpinzani wake katika mbio za Ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara.Dhidi ya Coastal Union na jana kwenye chezo wa Dabi dhidi ya Yanga.