Ufufuko wa La Masia na utawala mpya wa Barcelona

Kwa mara ya kwanza baada ya kizazi cha Xavi Hernandez, Andres Iniesta, Sergio Busquets, Victor Valdes, Gerald Pique na Carles Puyol Barcelona imeanza na Wachezaji Watano kutoka kwenye kituo cha kulelea Wachezaji cha La Masia kwenye dimba la Santiago Bernabeu mchezo wa El Clasico dhidi ya Real Madrid.

Joan Laporta amefanikiwa kuifufua La Masia na kituo hiko kimeifufua Barcelona, Wachezaji saba wote wamezaliwa miaka ya 2000 walianza kwenye mchezo wa El Clasico na kuwatawala Wenyeji wao bila uwoga wowote.La Masia imerudisha utambulisho wa Barcelona chini ya Hansi Flick.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS