Washambuliaji na Vita ya kiatu cha Dhahabu Ulaya

Barani Ulaya kwa sasa Wachezaji Wanaongoza kwa ufungaji wa magoli kwenye ligi kuu Tano kubwa ni Washambuliaji wa kati. Mabadiliko ya Sayansi ya mpira wa miguu imepelekea kupoteza baadhi ya Wachezaji ambao walisifika kwa kutimiza majukumu yao yaliyokuwa yanawaweka ndani ya uwanja.Mabadiliko wa kiucheza na mifumo mipya kwenye mpira wa miguu imepelekea kuibuka kwa Wachezaji wa pembeni yao Mawinga kutumika kama Washambuliaji wa kati na kumfanya namba Tisa ili aweze kucheza awe na sifa ya kuchezesha wengine kama kiungo wa kutokea juu yaani inside Forward. Harry Kane, Karim Benzema na Robert Firmino ni mfano sahihi wa Washambuliaji wa kati wenye uwezo wa kuchezesha wengine ndani ya uwanja.

Vita ya ufungaji bora barani Ulaya kwa sasa ni kubwa kutokana na uwepo wa namba 9 wenye uwezo mkubwa kutumia nafasi zinazotengenezwa na timu zao. Harry Kane ameshafunga goli 8 nchini Bundesliga, Erling Haaland ameshafunga goli 10 EPL, Robbert Lewandoski amefunga goli 12 msimu wa 2024-2025.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS