Mama na mtoto wafariki ajalini wakitoka chuoni
Mama mwenye umri wa miaka 35 na mtoto wake wa miezi 10, wamepoteza maisha baada ya kukanyagwa na gari wakiwa kwenye bodaboda eneo la mtaa wa Nguzo Nane, Manispaa ya Shinyanga akitokea Morogoro kufuata vyeti vyake Chuo Kikuu cha Mzumbe huku mwendesha bodaboda akitokomea kusikojulikana.