Wawili wafariki katika machimbo Arusha
Watu wawili waliotambulika kwa majina ya Baraka Mollell na Enock Lembris wamefariki na mmoja akijeruhiwa baada ya kuangukiwa na kifusi katika machimbo ya moramu ya mgodi wa Ngurumausi uliopo katika kata ya Muivaro jijini Arusha.