Diego Forlan kucheza mashindano ya tennis ya ATP

Nahodha wa zamani wa Uruguay na Mchezaji wa klabu ya Manchester United ya England atashiriki mashindano ya Tennis yatakayofanyika Uruguay Montevideo. Forlan ana umri wa miaka 45 atashirikiana na Federico Coria kwenye michezo ya wawili kwa wawili.

Nyota wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Uruguay Diego Forlan anashika nafasi ya 108 kwenye orodha ya Shirikisho la Tennis Duniani kwa Wacheza Tennis wenye umri wa miaka 45 na zaidi. Foralan aliwahi kucheza tennis kabla ya kuchagua mpira wa miguu kama mchezo wake pendwa.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS