Kocha wa zamani Simba SC asaini Al Ahly Tripoli

Kocha wa zamani wa klabu ya Simba amesaini mkata wa kuitumikia timu ya Al Ahly Tripoli ya nchini Libya. Didie Gomes Da Rosa alikuwa akifundisha timu ya taifa ya Botswana kabla ya kujiuzulu nafasi yake na kutangazwa kwenye klabu hiyo ya Libya kuwa Kocha wao mkuu. Gomes raia wa Ufaransa alishinda taji la ligi kuu Tanzania bara, kombe la shirikisho Tanzania ( FA ) na aliiwezesha klabu ya Wekundu wa Msimbazi kucheza hatua ya robo fainali kombe la klabu bingwa Afrika msimu wa 2021.

Didie Gomes Da Rosa ni Kocha mwenye uzoefu mkubwa na mpira wa Afrika, alishawahi kushika nafasi ya tatu katika tuzo za Zarpa Awards Makocha bora wa Kifaransa waliopo Afrika mwaka 2015, Al Ahly Tripoli imemuajiri Da Rosa baada ya kumfuta kazi raia wa Tunisia Chokri Khatoui.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS