Thomas Tuchel apewa miezi kumi na nane England

Thomas Tuchel kocha wa zamani wa Chelsea ya England amesaini mkataba wa miezi 18 kuiongoza timu ya taifa ya England. Kikosi hicho mabingwa wa kombe la Dunia mwaka 1966 kilikua chini ya Kocha wa muda Lee Carsley baada ya aliyekua Mkufunzi mkuu wa timu hiyo Gareth Southgate kujiuzulu mwezi Julai 2024. Tuchel anakuwa Mwalimu wa tatu ambaye si raia wa Uingereza kuiongoza England baada ya Sven- Goran Eriksson na Fabio Capello. Mjerumani huyo aliyewahi kushinda tuzo ya Kocha bora Ulaya na Dunia mwaka 2021 atasaidiwa na Antony Barry aliyefanya naye kazi Chelsea na Bayern Munich.
Thomas Tuchel koch wa zamani wa Chelsea aliiongoza klabu ya The Blues kushinda kombe la klabu bingwa Ulaya pamoja na kombe la klabu bingwa Dunia msimu 2020-2021. Mafanikio hayo na timu hiyo ya Jiji la London yalimpa tuzo ya Kocha bora wa Ulaya na Dunia mwaka 2021.