Waliosimamia ujenzi wa VETA Uyui kukamatwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Tabora, Musa Chaulo kuwakamata watu wote wanaohusika na usimamizi wa ujenzi wa chuo cha ufundi stadi (VETA) Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha.