Mshtakiwa kesi ya Zumaridi aanguka mahakamani
Kesi namba 12 inayomkabili Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi, na wenzake 84 ya kufanya mkusanyiko usio halali imelazimika kusimama kwa muda wa nusu saa baada ya mshtakiwa namba 74 aitwaye Neema Juma kuanguka akiwa kizimbani.