Sakata la abiria kushushwa Mbezi latua kwa Waziri
Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa, amemuagiza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, kukutana na wadau na wamiliki wa mabasi ili kuweka utaratibu mzuri ambao ni shirikishi wa utoaji huduma kwa wananchi kwenye kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli jijini humo.