Mwigulu aomba Rais Samia aendelee kuombewa
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Mwigulu Nchemba, ameziomba taasisi za dini kuendelea kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan, ili aendelee kuiongoza nchi vizuri na kutimiza dira yake ya uwekezaji katika sekta ya uzalishaji, kutengeneza ajira, kukuza uchumi na kujenga Tanzania yenye umoja.