Waziri Mkuu ataka nguvu zaidi uwezeshaji wananchi
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wadau wote wa uwezeshaji wananchi kiuchumi waongeze nguvu katika kutoa huduma za uwezeshaji hasa maeneo ya pembezoni ya miji na vijijini ili kufikia malengo ya nchi katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

