Mshtakiwa kesi ya Zumaridi aanguka mahakamani
Kesi namba 12 inayomkabili Diana Bundala maarufu kama mfalme Zumaridi na wafuasi wake 84 ya kufanya mkusanyiko usio halali leo hii imeshindwa kuendelea baada ya mshtakiwa namba 38 aitwaye Maria Julius kuanguka ghafla mahakamani na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu

