Jimboni kwa Simbachawene kupata maji
Wananchi wa Kata ya Pwaga, jimbo la Kibakwe mkoani Dodoma, wanatarajia kuanza kunufaika na mradi mpya wa maji baada ya serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa maji kupitia Mkandarasi Pioneer Building Limited.

