Wanafunzi wapewa tuzo kupunguza utoro
Katika kuhakikisha tatizo la utoro kwa wanafunzi linadhibitiwa na kuwezesha kufaulu mitihani yao, wanafunzi saba kutoka katika shule sita za msingi za serikali zilizoko kata Kanyangereko wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera, wamepatiwa tuzo ya fedha, medali na makombe, baada ya kufaulu.

