Tanzania yapokea bilioni 23.7 kutoka Ujerumani
Serikali ya Tanzania imesaini makubaliano ya shilingi bilioni 23.7 ya ushirikiano na serikali ya shirikisho la Ujerumani kwa ajili ya kudhibiti uharibifu wa wanyamapori na vifo vinavyosababishwa na wanyamapori kama Tembo katika jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi.