‘Panya road’ 100 wakamatwa Temeke
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo amesema ndani ya siku mbili zaidi ya wahalifu 100 wamekamatwa wakiwemo vijana wanaojiita ‘panya road’ ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo mbalimbali vya uhalifu wa kuvamia nyumba na kupora mali pamoja na kuwajeruhi watu.

