RUWASA waagizwa kuwasimamia wakandarasi
Wakala wa usambazaji maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA Wilaya ya Morogoro imeagizwa kuhakikisha inawasimamia kikamilifu wakandarasi wanaotekeleza miradi nane ya maji yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 30 wilayani hapo ili ikamilike kwa wakati.

