Mwalimu afungwa maisha kwa kulawiti mwanafunzi
Mwalimu wa shule ya msingi Kyawazaru, iliyopo wilayani Butiama mkoani Mara, Idrisa Athuman Najela, amehukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya wilaya ya Musoma, baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mwanafunzi.

