"Watoto wengi hawaelewi wanachofundishwa" - TET
Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kufanya mapitio ya mitaala ya elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu ikiwa ni utekelezwaji wa jukumu la msingi la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), ambayo hufanyika kila baada ya mzunguko mmoja wa elimu kukamilika.