RC Chalamila aagiza mkandarasi aongeze mafundi
Mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila amemuagiza mkandarasi wa kampuni ya Sure Civil and Building Contractors Limited, anayejenga shule ya sekondari ya wasichana ya Kagera River kuongeza idadi ya mafundi ili ujenzi huo ukamilike mwezi Desemba mwaka huu, kwa mujibu wa mkataba