Wafanyakazi viwandani wapewe mikataba - Ndalichako
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewataka wamiliki wa viwanda nchini kutekeleza ipasavyo sheria za kazi ikiwemo kuwapa mikataba ya kazi wafanyakazi wanaowaajiri ili kuepukana na migogoro mahali pa kazi.