Wamaasai 8 waliomshambulia Askari jela miezi sita
Vijana 8 wa jamii ya kifugaji ya Maasai, Kiteto mkoani Manyara, waliomshambulia kwa marungu Askari wa Jeshi la Polisi Kata ya Njoro, Inspekta Patrick, wamehukumiwa kwenda jela miezi sita ama kulipa faini ya shilingi elfu 50 na fidia ya laki 1 kwa kila mmoja.

