Ubadhirifu wa milioni 470 wanukia Manyara
Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa, amemuagiza Mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere, kufuatilia tuhuma za ubadhirifu wa shilingi milioni 470 zilizojitokeza katika ujenzi wa shule ya sekondari Matui mkoani humo, baada ya yeye kutoridhishwa na ujenzi huo pamoja na kubaini mapungufu.