Watu 54 wathibitika kuugua Surua nchini
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kwamba kuna ongezeko la wagonjwa wa Surua nchini, ambapo sampuli zilizochukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa ugonjwa wa Surua zimeonesha halmashauri 7 zina mlipuko wa ugonjwa huo na kufanya waliothibitishwa na ugonjwa huo kuwa ni 54.
