Mwalimu atuhumiwa kulawiti wanafunzi wanne
Mwalimu wa shule ya msingi Kyawazaru Idrisa Athumani (29) mkazi wa wilayani Butiama mkoani Mara, amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za ulawiti wa wanafunzi wanne katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma na kusomewa mashtaka manne kwa mahakimu wanne wa Mahakama hiyo.