Dkt. Mpango ahimiza utunzaji wa bahari

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo (Kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makala (Kulia) wakati akiondoka katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere uliopo Jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua Warsha ya Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya usimamizi wa mazingira ya Bahari leo tarehe 19 Julai 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 19 Julai 2022 amefungua warsha ya Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini, usimamizi na utunzaji wa mazingira ya Bahari.