Watoto mkoani Mtwara wadaiwa kukosa malezi
Katibu Tawala wilaya ya Mtwara Thomas Salala, amesema kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa wakikwepa majukumu ya kulea watoto wao na badala yake watoto wengi kulelewa na bibi na babu, hali ambayo husababisha watoto kukosa upendo na kuleta madhara kwa Taifa na jamii kwa ujumla.