Madalali wachangishana kujenga kituo cha afya
Umoja wa madalali zaidi ya 30 wa Kata ya Iwungilo, Halmashauri ya Mji Njombe, wameamua kuchangia ujenzi wa kituo cha afya ambacho kinatarajia kuanza ujenzi wake mapema mwezi huu ili kuwanusuru wananachi ambao mpaka sasa wanafuata huduma umbali mrefu.
