"Ratiba ya kufungua shule iko vilevile" - Waziri
Serikali imekanusha uzushi uliotolewa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema na sekta ya elimu kwa kusema shule nchini zitafunguliwa Septemba 21 jambo ambalo si sahihi na wala hakuna muongozo wala maelekezo hayo.

