Serikali kuanzisha ufadhili wa masomo ya sayansi
Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ipo kwenye hatua za mwisho za kuanzisha ufadhili wa masomo ya sayansi (SAMIA SCHOLARSHIP) kwa wanafunzi wenye ufaulu mzuri kwakuwa Rais tayari ametoa fedha nyingi zinazoweka msukumo wa masomo ya sayansi kwa wanafunzi wote Tanzania

