"Endelezeni Utii na Weledi" - Dkt. Stergomena Tax
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb), amewataka watumishi wa Wizara ya Ulinzi na JKT kuendeleza utii, weledi na uaminifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi, na kuepuka migogoro mahali pa kazi.