Dkt. Mollel amsimamisha kazi Mhandisi
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, amemsimamisha kazi mkuu wa idara ya ujenzi na msimamizi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Ukerewe mkoani mwanza Mhandisi Paul Koroso kwa kushindwa kutoa mchanganuo wa matumizi ya fedha za ujenzi huo ambazo ni shilingi bilioni 2.7.