Wadau wa utalii watakiwa kuchangamkia fursa
Wadau wa utalii hususani wakala wa biashara za utalii, watoa huduma za malazi, wakala wa safari na waongoza watalii wametakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi zitakazotokana na onesho la Swahili International Tourism Expo (S!TE) litakalofanyika Dar es Salaam Oktoba 21 hadi 23, 2022.