Upasuaji wa moyo bila kuongeza damu waanza JKCI
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kukwete (JKCI) imekuja na teknolojia mpya ambayo inamfanyia upasuaji mgonjwa wa moyo bila ya kumuongezea damu kama ilivyokuwa inafanyika awali. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi.