Waliohamia Msomera waishukuru serikali

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza, Bw. Richard Tobiko Ole Makoro (kulia) ambaye ni mmoja wa wakazi wapya wa kijiji cha Msomera wilayani Handeni Mkoa wa Tanga waliohamia katika kijiji hicho kutoka Ngorongoro wakati alipofika nyumbani kwa mkazi huyo kujionea mazingira anayoishi, Juni 23, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wakazi wapya wa kijiji cha Msomera, Handeni Mkoani Tanga waliohamia kutoka Ngorongoro wameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya huduma za jamii katika eneo hilo.