"Hakuna sababu akina Halima kuwa bungeni"- Mnyika
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali kesi ya msingi iliyokuwa imefunguliwa na wabunge 19 akiwemo Halima Mdee, waliovuliwa uanachama na chama cha CHADEMA hivyo kuruhusu taratibu zingine kuendelea.