"Watu wanavunja sheria za uhifadhi makusudi"-Chana
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana, amesema wapo watu wachache wanaovunja sheria za uhifadhi kwa makusudi na wengine kwa kutokujua sheria, hasa wafugaji wanaoingiza mifugo kwenye Hifadhi za Taifa na mapori ya akiba yaliyo kwenye Kanda ya Kusini.