Mawakili wa Mfalme Zumaridi waomba ahamishwe
Mawakili wa upande wa utetezi katika inayomkabili Mfalme Zumaridi na wenzake wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kama itawezekana mteja wao awekewe ulinzi au ahamishwe katika Gereza Kuu la Butimba alililopo hivi sasa kufuatia kuwepo kwa taarifa za kuuawa kwake ndani ya gereza.