Polisi kuwasaka waliomuua Padre na mwili kuutupa
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya, limetangaza msako kwa wahusika wote wa mauaji ya Padre wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya, Michael Samson (63), Raia wa Malawi, kilichotokea kwenye mazingira ya kutatanisha baada ya kutoweka na mwili wake kupatikana maeneo ya Sabasaba kando ya mto Meta.