.jpg?itok=bOG6pNIm×tamp=1473366446)
Aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chma cha ADC na mwanasiasa mkongwe nchini Hamad Rashid, ameitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC kuangalia utaratibu mzuri wa kuondoa sintofahamu za kukiukwa kwa sheria zinazojitokeza katika chaguzi nchini pamoja na vyombo vya usalama kuacha kuwa sehemu ya siasa.
Bw. Rashid ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati ADC ikitangaza msimamo wa wao na kusema kuwa chama hicho kitashiriki katika uchaguzi wa marudio Zanzibar uliotangazwa kufanyika Machi ishirini..
Mbali na kuwatakia heri wananchi wa Zanzibar kujiandaa kwaajili ya kufanya uchaguzi ametoa wito kwa tume ya uchaguzi kusimamia uchaguzi kwa haki na kuwataka kutoyumbishwa na wanasiasa katika kufanya maamuzi.