Sunday , 1st May , 2016

Chama cha ADC Dira ya Maendeleo nchini Tanzania kimeiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama Siasa nchini ifanye uchunguzi wa kina kuhusu mgogoro unaondelea ndani ya chama hicho.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Dira ya Maendeleo, Bw. Doyo Hassan Doyo akionyesha baadhi ya nyaraka za chama hicho mapema leo jijini Dar es salaam.

Chama cha ADC Dira ya Maendeleo nchini kimeiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama Siasa nchini ifanye uchunguzi wa kina kuhusu mgogoro unaondelea ndani ya chama hicho baina ya uongozi wa chama na Mmwenyekiti wa chama hicho Bw. Saidi Miraji.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Dira ya Maendeleo, Bw. Doyo Hassan Doyo alipokua akizungumza na waandishi wa habari juu ya mgogoro unaondelea ndani ya chama hicho cha siasa na kusema kuwa kuna baadhi ya wanachana wamekuwa wakipotosha Ofisi ya Msajili wa vyama na kupelekea ofisi hiyo kufanya kazi kwa matabaka.

Wakati huo huo uongozi wa ADC wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kufanya maamuzi kwa kuzingatia sheria kwani kunaweza kukawa na tabia yakusingiziana makosa ili mtu aadhibiwe.