Tuesday , 3rd May , 2016

Polisi nchini India wamesema kuwa kijana Mmoja amejipiga risasi kichwani kwa bahati mbaya wakati akijaribu kujipiga picha ya 'Selfie' akiwa ameshikilia bunduki iliyokuwa ikimilikiwa na baba yake.

Jinsi ya watu wanavyojishughulisha na picha za Selfie

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 15 anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Pathnkot iliyopo katika Jimbo la Punjab.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa kijana huyo alichukua bastola ya baba yake lakini kwa bahati mbaya alijipiga risasi kichwani akitaka kupiga picha ya 'Selfie' akiwa ameshika bastola kichwani.

Tukio hilo limevuta hisia kali miongoni mwa watu nchini humo, ambao bado wanaomboleza kifo cha kijana mwengine aliyekanyagwa na treni wakati akijaribu kupiga picha ya 'Selfie' kwenye reli wakati treni ikipita kwa kasi.

Takwimu zinaonyesha kuwa katika kila vifo 27 vya watu vilivyotokea kote duniani mwaka jana vilitokana na picha za 'Selfie'.