Sunday , 10th Jan , 2016

Asasi za kiraia nchini (AZAKI), wametoa tamko kuwataka wanasiasa Visiwani Zanzibar kuwa na utaratibu kutolewa taarifa ya maendeleo ya majadiliano yanayofanywa na viongozi wanaokutana kuhusu suala la muafaka wa kisiasa Visiwani humo.

Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Asasi za Kiraia(NACONGO)Bw. Onesmo Ole Ngurumwa

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Asasi za Kiraia(NACONGO) Bw. Onesmo Olengurumwa amesema kuwa ili kuinisuru Zanzibar ni lazima viongozi hao waweke utaratibu wa kuwajulisha wananchi ya juu kinachoendelea.

Olengurumwa ameongeza kuwa viongozi hao wajikite zaidi katika kuzingatia sheria na katiba wanapokusudia kufanya maamuzi ya utatuzi wa mgogoro wa kisiasa Zanzibar kinyume na hivyo watazua machafuko yasiyokuwa na ulazima.

Aidha Katibu Mkuu huyo amesema AZAKI inawataka viongozi wote watumie siku ya mapinduzi kuwatangazia wananchi hatma ya Zanzibar ya kisiasa kwa kuwa wazanzibari wanayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika uamuzi juu ya mambo yanayohusu taifa lao.

Aidha muungano huo wa asasi hizo za kiraia wamesema kuwa viongozi wanaojadiliana kuhusu muafaka huo wameshapata muda wa kutosha na kwamba sasa ni muda wa kuwaambiwa wananchi juu ya maswali ya ajenda zao wamefikia wapi, wamebakiza wapi, na lini watamaliza majadiliano yao na lini watatoa tamko la muafaka wa kumaliza mgogoro