
Mkulima wa ngano wilayani Monduli akionesha hali ya kilimo hicho mkoani Arusha.
Kwa mujibu wa FAO, mtizamo wa mwanzo unaonyesha nafaka kuu, zipo katika nafasi ya kushusha gharama za uagizwaji wa chakula kwa miaka sita.
Rekodi za utabiri wa uzalishaji kimataifa za mwaka huu kwa uvunaji wa ngano na mchele pamoja na kuongezeka kwa kipato cha mahindi zinasaidia utoshelevu na kushuka kwa bei.
FAO inasema kuwa kote duniani kiwango cha uzalishaji wa nafaka kwa mwaka 2016 kinapaswa kuongeza tani zaidi ya milioni mbili hadi asilimia moja na nusu kutoka katika kipindi cha mwaka uliopita.