
Jenista Mhagama
Waziri Muhagama amesema kuwa endapo kima cha chini cha mshahara kisiposimamiwa vyema kinaweza kusababisha migogoro isiyo ya lazima na kuchangia kuzorotesha shughuli za maendeleo za wananchi.
Uzinduzi huo wa bodi ya mshahara ulifanyika mjini Dodoma ambapo Waziri Jenista alitumia hotuba yake hiyo kusema kuwa kima cha chini kisipozingatiwa kinaweza kuzorotesha maendeleo ya nchi uwekezeji na biashara katika nchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya Mishahara katika sekta ya Umma Getrude Mlaka, ameahidi kuwatendea haki watumishi wa umma huku mwenyekiti wa bodi wa kima cha chini cha mshahara sekta binafsi Mkumbuka Philmon akiahidi kutokufanya kazi kisiasa.
Kuzinduliwa kwa bodi ya mishahara kumepeleka kufutwa rasmi kwa utitiri wa bodo zilizokuwa ziki shughulika kulingana na kada na sekta mbalimbali.