Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

'CCM imedhulumiwa sana' - Rais Magufuli

Tuesday , 22nd May , 2018

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli, amesema kwamba mali za Chama hicho zimeibiwa kwa kiasi kikubwa  kutokana na usimamizi mbovu ulikuwa unafanywa na watendaji wa chama hicho.

Rais Magufuli amesema hayo Mei 21, 2018 katika Ofisi ndogo za CCM, Lumumba Jijini Dar es salaam baada ya kupokea Ripoti ya Tume ya kuhakiki mali za CCM nchi nzima na kuongeza kuwa haiwezekani Serikali inapambanua na ufisadi wakati chama tawala hakioneshi mfano kupinga ubadhirifu.

“Ripoti imesheheni mambo mengi, CCM imedhulumiwa kweli, inaumiza sana mpaka nimechoka, lakini ndiyo hivyo nimeipokea lengo ni kuhakikisha tunakuwa na chama ambacho matumizi ya fedha na miradi inayosimamiwa na chama iwe miradi ya ukweli na isiwe ya utapeli” amesema Rais Magufuli

Rais Dkt. Magufuli ameongeza kwamba ripoti hiyo ataiwasilisha kwa wajumbe wa mkutano wa Halmashuri kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC) ili kuijadili ripoti hiyo na badae kutoa maamuzi kutokana na malekezo ya wajumbe hao.

Disemba 20, 2017 katika kikao cha Halmashauri kuu CCM (NEC) Rais John Magufuli aliunda tume ya wajumbe tisa wakiongozwa na mwenyekiti Dkt. Bashiru Ali Kakurwa ambapo tume hiyo ilipewa jukumu la kuhakiki mali za Chama nchi nzima kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa.
 

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine